Wanajeshi na polisi wamekuwa wakishika doria maeneo mengi Ufaransa |
Azimio hilo lililotayarshwa na Ufaransa linahimiza mataifa yote wanachama wa UN “kuchukua hatua zote zifaazo” kukabiliana na IS.
Kundi la IS lilisema lilihusika kwenye mashambulio hayo ya Paris yaliyosababisha vifo vya watu 130.
Aidha, lilidai kuhusika katika kulipua mabomu Lebanon mwezi huu. Awali, lilikuwa limesema lilihusika kudungua ndege ya Urusi eneo la Sinai mwezi Oktoba, na kuua watu 224.
Azimio hilo la UN nambari 2249 linashutumu mashambulio ya hivi majuzi Sousse, Tunisia, na Ankara, Uturuki
Mgahawa wa Carillon ni miongoni mwa maeneo yaliyoshambulia Paris, na hapa maua yanaonekana kwenye shimo lililotobolewa na risasi |
Hatua hiyo ilichukuliwa huku maafisa nchini Ubelgiji wakitangaza kiwango cha juu zaidi cha tahadhari Brussels, na kuonya huenda kukatokea shambulio.
Baadhi ya walioshambulia Paris walikuwa wamekaa Brussels. Manusura pekee wa kundi hilo, Salah Abdeslam, bado anasakwa na anadaiwa kurejea humo.
Serikali ya Ubelgiji imesema mshukiwa mwingine ameshtakiwa kuhusiana na mashambuliano hayo, na kufikisha idadi ya walioshtakiwa nchini humo hadi watatu.
Usalama umeimarishwa nchini Ufaransa |
Azimio hilo pia linasisitiza kwamba mataifa yanafaa “kuongeza maradufu na kuendesha juhudi za kuzuia na kukabili mashambulio ya kigaidi kwa pamoja”.
Hata hivyo, haijagusa Sura VII ya UN ambayo huidhinisha kutumiwa kwa nguvu.
Ufaransa na Urusi zilisema tayari inaruhusiwa kutumia nguvu kwa sababu mataifa yana haki ya kujilinda.
Awali, maafisa wa Ufaransa walisema binamu wa mhusika mkuu wa mashambulio hayo ya Novemba 13 mjini Paris hakujilipua wakati wa operesheni ya polisi Saint Denis kama ilivyodhaniwa awali.
0 comments:
Post a Comment